MTOTO WA MIAKA MIWILI KUINGIZWA NDANI YA KISIMA

 

Kumeripotiwa tukio la kifo cha mtoto wa miaka miwili kuingizwa ndani ya kisima maeneo ya tomondo uzi na mtu asiyefahamika.

Tukio hilo la kusikitisha limemkuta mtoto huyo mkaazi wa tomondo ambapo kabla ya kukutwa na mkasa huo, kwa mujibu wa maelezo ya watoto wenzake ambao walikuwa wanacheza pamoja, alitokea mwanamke asiyefahamika na kumchukuwa mtoto huyo.

Muda mfupi maiti ya mtoto huyo ikakutwa ndani ya kisima wakati mkaazi mmoja wa eneo hilo akiwa katika harakati za kuchota maji kama anavyoeleza.

Kufuatia tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi amethibitisha kutokea mkasa huo na polisi inaendelea na uchunguzi kubaini aliehusika na tukio hilo.