MTOTO WA TRUMP AJITETEA KUHUSU MAWASILIANO NA URUSI

Mtoto mkubwa wa kiume wa rais wa marekani donald trump, amesema wakili wa urusi aliyekutana naye hakufichua habari kuhusu mgombea wa urais wa democratic hillary clinton.
Katika mahojiano na televisheni ya fox, donald trump junior, amekanusha kuwa mkutano wake na wakili wa urusi natalia veselnitskaya wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais wa 2016 ulikuwa na habari kumhusu clinton.
Ufichuzi wa barua pepe inayomhusisha trump junior. Umekuja wakati ambapo uchunguzi unaendelea nchini marekani kuhusu timu ya kampeni za trump kushirikiana na urusi katika jaribio la kushawishi matokeo ya uchaguzi wa rais nchini humo mwaka jana.