MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA NA WENGINE ISHIRINI NA TANO WAMEJERUHIWA

 

 

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine ishirini na tano wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya kiashange matwemwe mkoa wa kaskazini unguja.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 3 asubuhi baada ya  dereva makame seif juma kushindwa kuimudu gari  aina ya towne haice aliyokuwa akiiendesha kwa mwendo wa kasi  na kupinduka katika maeneo ya kiashangwe na kusababisho kifo cha mtu mmoja alietambulika kwa jina la mwajuma pandu simai.Baadhi ya majeruhi waliopatikanwa katika ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya mnazi mmoja na wengine wamelazwa katika hospitali ya kivunge .

Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini unguja hasina ramadahan taufik amesema gari hiyo iliyokuwa imepakia abiria  kwa mujibu wa sheria haikustahiki kupakia abiria hivyo kufanyahivyo ametenda kosa kisheria.Nae daktari dhamana wa hospitali ya kivunge maulid abdalla khamis amesema hali za majeruhi zinaendelea vizuri huku wakiendelea kupatiwa matibabu.Mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja vuai mwinyi moh’d amewasisitiza madereva kuacha tabia ya kujaza abiria kupita kiasi na kuacha kuendesha gari kwa mwendo wa  kasi .