MTU MMOJA AMENUSURIKA KUFA KWA KUTUMBUKIA KISIMANI

 

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la maryam hassan  ndundu mwenye umri wa miaka 48 amenusurika kufa baada ya kuingia katika kisima cha mkata huko shehia ya kiongoni makunduchi wilaya ya kusini.

Kunusurika kwa mtu huyo kumetokana na jitihada za wananchi wa eneo hilo baada ya kupata taarifa ya mama huyo kuingia kwenye kisima ni mara ya pili kumtokezea tukio hilo ambae anasadikiwa ni mgonjwa wa akili.

Wakisimulia juu ya tukio hilo mashuhuda wamesema mtu huyo ambae amejitia katika kisima hicho majira ya saa tisa alaasiri alikuwa akitokea nyumbani kwao kijiji cha roho mbaya na kufika maeneo hayo kujitumbukiza hivyo wamefanikiwa kumuokoa akiwa hai na hatimae  kukimbizwa katika hospitali ya cottage makunduchi kwa kupata matibabu na uchunguzi zaidi.

Akiwa katika eneo la tukio mkuu wa wilaya ya kusini mhe idrissa kitwana mustafa amewashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa mashirikiano na ujasiri mkubwa waliouonyesha katika kuokoa uhai wa mama huyo na kuwataka wananchi kuwa na tahadhari kwa kuwa nao karibu watu wenye matatizo ya akili ili kuepukana na matatizo kama hayo yanayoweza kujitokeza.

Hata hivyo amesema serikali wilayani humo itachukua hatua ya kukifunika kisima hicho kwa vile hakitumiki ili kuepusha maafa