MUGABE HANA MIPANGO YA KUACHIA MADARAKA

 

Mugabe ambaye kesho anatimiza umri wa miaka 93, amesema hakuna mtu anaekubalika anayeweza kumrithi.

Kiongozi huyo ambaye ameiongoza zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1980, ameendelea kukanusha taarifa kwamba ana matatizo ya kiafya.

Uchumi wa zimbabwe umeyumba wakati wa utawala wa mugabe na miezi ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la mfumko wa bei pamoja na uhaba wa fedha.