MUSEVENI ATAKA KUIDHINISHA MISWADA YA KUOMBA MIKOPO

Museveni ataka kuidhinisha miswada ya kuomba mikopo

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemwandikia barua spika wa Bunge Rebecca kadaga kuhakikisha mikopo yote ya serikali imfikie kabla ya kujadiliwa bungeni.

Museveni ameelekeza kuwa mikopo 11 ya serikali iliyopelekwa bungeni ikataliwe kwa sababu haisadii kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

aidha, ameruhusu maombi 16 ya mikopo kupitishwa kwa sababu inalenga kuimarisha miundo mbinu kama ya barabara pamoja na kuinua sekta ya afya na elimu nchini humo.

kufikia mwisho wa mwaka uliopita, Uganda ilikuwa na Deni la Dola bilioni 8.7.