MWAKILISHI KUWAJENGEA WANANCHI WAKE BARABARA YA KIWANGO CHA FUSI KATIKA KIJIJI CHAO

 

 

wananchi wa kijiji cha ngoma hazingwa wilaya ya chake chake wamemshukuru mwakilishi wa jimbo lao nd suleiman said sarahan kwa kuwajengea barabara kwa kiwango cha fusi katika kijiji chao.

wananchi hao wametoa shukrani  hizo  wakati walipokua wakizungumza na zbc huko kijijini kwao na kusema kuwa barabara hiyo itawarahisishia katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kuondokana na changamoto ya umasikini.

nd suleiman amesema ameamua kufanya hivyo kutokana n kadhia inayowakumba wanakijiji hao katika shughuli zao za kila siku jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo hususa akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

pia amefurahishwa na ushirikiano wa wanakijiji hao mfano kwa kutoa vipando vyao bila ya malipo yoyote jambo ambalo ni mfano wa kuigwa kwa wananchi hao.