MWAMKO WA JAMII UNAHITAJI KUONGEZWA KATIKA KUCHANGIA DAMU

 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja dk. Idrissa Muslih hija amesema mwamko wa jamii unahitaji kuongezwa katika kuchangia damu ili kuondosha usumbufu wa upatikanaji wa huduma hiyo.

Amesema hiyo itafanikisha kupatikana damu ya kutosha kwenye benki ya damu itakayokidhi mahitaji wagonjwa hasa wa dharura.

Akizindua zoezi la uchangiaji damu kwa mkoa wa kusini liloandaliwa na kundi la g1 amesema suala la uchangiaji damu kwa mwananchi liwe la hiari kwani wataokoa maisha ya watu hasa wanaopatwa na ajali na wajawazito.

Wakaazi wa maeneo mbali mbali ya mkoa huo walioshiriki zoezi hilo wametoa wito kwa wananchi wengine kuwa na mwamko wa kuchangia damu badala ya kuiachia wizara ya afya pekee kwani kuna matatizo mengi ya akiafya ambayo yanahitaji huduma hiyo.

Afisa uhamasishaji benki ya damu zanzibar dk. Bakari hamad amesema katika kipindi kijacho cha mwezi wa ramadhani mahitaji ya damu yanaongezeka kutokana na kuwepo kwa ajali nyingi hivyo hali hiyo itasaidia kuokoa maisha ya wananchi.