MWANAHARAKATI ALIYEPIGA VITA UBAGUZI WA RANGI AFRIKA KUSINI AFARIKI DUNIA.

 

Kiongozi mwanaharakati aliyeshiriki kupigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Ahmed Kathrada amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87.

Kathrada alifariki dunia akiwa katika hospitali moja mjini Johannesburg baada ya kuugua kwa muda mfupi kufuatia upasuaji aliofanyiwa kwenye ubongo.

pamoja na Nelson Mandela, kathrada alikuwa miongoni mwa wanaharakati wanane wa African National Congress waliohukumiwa kufungwa jela maisha mwaka 1964.

walipatikana na hatia ya kujaribu kupindua serikali ya ubaguzi wa rangi na alikaa jela miaka 26 kabla ya kuachiwa huru mwaka 1989 ambapo rais Mandela baadaye alimshawishi kujiunga na serikali.