MWANAKWEREKWE KUKERWA NA UCHAFU WA KUTUPWA VINYESI KATIKA MAENEO YAO

 

Wakaazi wa shehia ya Ijitimai Mwanakwerekwe wameelezea kukerwa na uchafu wa kutupwa vinyesi katika maeneo yao jambo ambalo linahatarisha usalama wa afya zao.

Wamesema tabia hiyo ipo kwa muda mrefu na inafanywa na watu wasiozingatia maadili na kulinda afya za watu wengine na kuziomba taasisi zinazohusika kuwasaidia kukomesha vitendo hivyo.

Wananchi hao wameiambia zbc kwamba  hali hiyo imewafanya kuishi kwa hali ya wasi wasi katika makaazi yao wao na familia zao kutokana na kushamiri kwa vitendo viovu ambavyo vinafanywa  zaidi   nyakati za harakati za asubuhi.

wamesema mbali ya tabia hiyo pia waendesha gari za abiria wamekuwa wakitumia maeneo ya   makaazi yao  kwa kuweka gari bila ya kutumia maeneo waliyopangiwa.

bibi fatma massoud othman ni naibu sheha wa shehia  ijitimai    amekiri kuwepo kwa tabia hiyo   na kuahidi  kuvichukua hatua za  kisheria vitendo hivyo.

kutokana na kujitokeza kwa tabia  hiyo watu wanao tafuta  chupa kwa ajili ya kufanyia biashara wanapaswa kuwa na tahadhari kwa kuhofia afya zao na za watu wengine.