MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI WA ZBC MAREHEMU MARIDADI AMANI AZIKWA

 

Mamia ya wananchi wakiwemo viongozi wa serikali wameshiriki mazishi ya mwandishi wa habari mwandamizi wa shirika la utangazaji zanzibar marehemu maridadi amani alioyefariki dunia jana.

Mazishi ya mwanahabari huyo aliyefia katika hospitali ya global yamefanyika kikijiji kwao ndunduke wilaya ya magharibi ‘a’.

Sala  na dua ya kumuombea marehemu huyo ilifanyika katika msikiti wa aman ikiongozwa na katibu wa mufti wa zanzibar shekh fadhil suleiman soraga.

Wananchi kadhaa wanaomfahamu marehemu maridadi akiwemo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya magharibi ‘b’ mwinyiusi  abdalla hassan wamemsifu maridadi kutokana na uhodari wa kazi yake sambamba na kushirikiana vyema na jamii katika masuala mbali mbali.

mafanyakazi wa shirika la utangazaji zanzibar kwa niaba ya mkurugunzi mkuu wanawaomba wafiwa kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu.

Marehemu aliyezaliwa mwaka 1975 na kusoma katika skuili ya ben bela ameacha watoto watatu mungu alilaze roho yake pahala pema peponi amin……..