MWENGE WA UHURU UMEWASILI LEO UNGUJA, BAADA YA KUMALIZA MBIO ZAKE KATIKA MIKOA MIWILI PEMBA.

mwenge wa uhuru umewasili leo kisiwani unguja, baada ya kumaliza mbio zake katika mikoa miwili ya kisiwa cha pemba.
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa abeid amani karume, mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mheshimiwa omar khamis othman, alimkabidhi mwenge huo kaimu mkuu wa mkoa wa kaskazini unguja, mheshimiwa ayoub mohammed mahamoud.
akisoma risala ya mkoa wa kaskzini pemba, mheshimiwa omar amesema mwenge wa uhuru umemaliza ziara yake katika hali ya usalama na kufanikisha vyema malengo yaliokusudiwa, ikiwemo uzinduzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na ushajihishaji wa masuala ya kijamii.
amesema jumla ya miradi 16 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 567 ilizinduliwa mkoani humo.
amesema kupitia mbio za mwenge wa uhuru, wananchi 76 walijitokeza kupima maambukizo ya virusi vya ukimwi, na kubainika wote wakiwa salama.
aidha amesema, kwa nyakati tofauti viongozi wa mbio za mwenge wa uhuru walipata fursa ya kuielimisha jamii na kuiasa juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya, mapambano dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na namna ya kukabiliana ugonjwa wa malaria.
mheshimiwa omar amesema mkoa wa kaskazini pemba, unaendelea na juhudi za kukabiliana na vitendo vyote vinavyokwamisha maedeleo na ustawi wa kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo.
mwenge wa uhuru unatarajiwa kumaliza ziara yake mkoa wa kaskazini unguja oktoba 9, mwaka huu na badaae kukabidhiwa kwa uongozi wa mkoa wa kusini unguja, kuendelea na mbio hizo.