MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI AMEWATAHADHARISHA VIJANA

 

 

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jecha Sali Jecha  amewatahadharisha vijana   kuwa makini  na uchochezi wa aina yoyote unaoweza kuwashawishi kuvuruga mipango ya serikali.

Akifungua semina kwa  makundi  maalum ya vijana amesema  mara nyingi vijana wamekuwa wakitumika kufanya vitendo ambayo baadae vinaweza kuwaletea madhara katika maisha yao.

Amewashauri vijana kujitathmini  kwa kile ambacho wanataka kukifanya  kwa kujifunza mambo muhimu kabla hawajachukua uamuzi wa jambo lolote, na kuwataka kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kufanyika mwezi 12 mwaka huu.

Akiwasilisha mada  ya  nafasi za vijana  katika maendeleo ya nchi,   katibu mtendaji  baraza la vijana  shaib  ibrahim  mohd amesema mbali na fursa zilizopo  katika kuwapatia maendeleo vijana  ni vyema  kuimarisha  utaratibu  wa mipango na sera  zinazohusiana na  maendeleo ya vijana  nchini.

Wakitoa maoni yao  vijana hao wameitaka tume ya uchaguzi  zec   kuwaandalia mbinu mbadala ambazo zitaisaidia jamii  kupata taarifa zinazomuhusu mpiga kura   kwa teknologia ya njia ya simu ili kuwaondoshea wananchi usumbufu  wa kuzijua tarifa zao