NCHI JIRANI ZILIZOIWEKEA VIKWAZO QATAR HAZINA NIA YA DHATI KUUMALIZA MGOGORO WA GHUBA

Wizara ya mambo ya nje ya qatar imesema nchi jirani zilizoiwekea vikwazo nchi hiyo hazina nia ya dhati kuumaliza mgogoro wa ghuba unaoendelea.
Akizungumza katika mkutano wa baraza la shura waziri wa wizara hiyo sheikh tamim bin hamad al thani amezitaja nchi za saudi arabia, umoja wa falme za kiarabu, bahrain na misri kuwa wamekataa mazungumzo na hawana nia ya kutaka suluhu juu ya kuutatua mgogoro huo.
Nchi hizo zimeiwekea vikwazo qatar mwezi june mwaka huu kwa kuituhumu kuwa inaunga mkono ugaidi na inajiweka karibu kwa kufunga mikataba na nchi ya iran madai ambayo yamekanushwa na qatar.
Sheikh al thani amesema nchi yake iko tayari kufanya makubaliano yanayokubalika kwa mustakabali wa nchi hizo lakini vikwazo walivyowekewa havina nia ya kutaka suluhu na vikwazo hivyo vinarudisha nyuma nguvu ya nchi na wananchi wa qatar.