NCHI ZA AFRIKA KUZINGATIA UTABIRI UNAOTOLEWA NA WAKALA WA HALI YA HEWA

Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano prof.makame mnyaa mbarawa, amesema ipo haja kwa nchi za afrika kuzingatia utabiri unaotolewa na wakala wa hali ya hewa ili kuinusuru jamii kukumbwa na majanga.

Waziri mbarawa  aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wataalamu utabiriwa hali hewa  kwa nchi za afrika  mashariki  .amesema  wakulima wengi wamekuwa wakitegemea mvua hivyo, utabiri wa hali ya hewa kwa ajili ya shughuli za kilimo utawasaidia kujipanga na kulima kwa kutegemea utabiri huo.

Proffesa mbarawa amesema utabiri wa hali ya hewa  hapa tanzania hasa kwa kipindi cha mvua kuanzia mwezi oktoba hadi disemba, utawapekea wananchi wanautumia kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amesema kumekuwepo na tabia miongoni mwa baadhi ya wananchi kupuuza taarifa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa  na baadaye kujikuta wakiathirika kwa sababu ya kutochukua tahadhari mapema.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa (tma), dk. Agness kijazia amesema mkutano huo utakuwa ukiangalia viasharia vyote vya kunyesha kwa mvua hizo mwaka huu kwa ajili ya maendeleo ya wanachi.

Amesema  katika kuhakikisha utabiri wa hali ya hewa unawafikia wananchi, tma imejipanga kuanza kutoa taarifa kupitia simu za mikononi ili kuweza kuwafikia kwa haraka zaidi.

Mkutano huo utalenga kurahisha mifumo ya hali ya hewa kwa njia rahisi zaidi kabla ya kuwafikia wananchi na kuzitumia vyema taarifa hizo mkutano huo wa 41 utaangalia mifumo ya hali ya hewa tanzania na pembe ya afrika .