NDEGE ZA MUUNGANO WA KIJESHI ZIMEFANYA MASHAMBULIZI YEMEN

Ndege za muungano wa kijeshi unaoongozwa na saudi arabia zimefanya mashambulizi dhidi ya ngome za waasi wa houthi mjini sanaa, nchini yemen baada ya rais wa zamani wa nchi hiyo ali abdullah saleh kusema yuko tayari kuufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na muungano unaoongozwa na saudi arabia, ikiwa muungano huo utasitisha mashambulizi nchini mwake.
Hatua hiyo inaweza kutengeneza njia ya kupatikana suluhisho la vita ambavyo vimedumu kwa takriban miaka mitatu.
Mabadiliko hayo yamejiri wakati wafuasi wa saleh wakipambana na wapiganaji wa houthi kwa siku ya tano katika mji mkuu wa yemen, sanaa.
Rais wa yemen anayetambuliwa kimataifa abd-rabbu mansour hadi pia amesema yupo tayari kufanya kazi na saleh dhidi ya waasi wa houthi ambapo muungano unaoongozwa na saudi arabia umekubali mabadiliko anayotaka kuyafanya saleh.