Blog

HALI YA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI BADO IKO JUU

Pamoja na kampeni mbalimbali kuhusu ugonjwa wa ukimwi zinazofanywa nchini, hali ya maambukizi ya ugonjwa huo bado iko juu hususani kwa vijana huku kundi la wasichana likiwa lipo juu.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na kaimu mkurugenzi mtendaji wa tume ya kudhibiti ukimwi tanzania (TACAIDS) Juma Isango wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za wasichana balehe na vijana kike tanzania.

Amesema maambukizi mapya kwa vijana ni aslimia 40 ambapo kati ya hizo wasichana ni asilimia 80.

Awali akifungua mkutano huo katibu mtendaji wa baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bi Beng’i Issa amewataka wasichana kujitambua na kujishughulisha na shughuli zauchumi, elimu ya afya ya jamii na rika ili waweze kuwa kioo cha jamii.

Mkutano huo umeshirikisha vijana wanawake kutoka mikoa tisa Tanzania bara na asasi za kiraia ukiwa na lengo la kutoa elimu kwa vijana kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

WATENDAJI WA MADARAKA YA UGATUZI WAMETAKIWA KUTAMBUA MAJIKUMU YAO

Watendaji wa madaraka ya ugatuzi wametakiwa kutambua majikumu yao, katika kuwafikishia wananchi huduma kwa lengo la kufikia dhamira ya serikali.

Kaimu Mkurugenzi Wa Baraza la Mji Chake Chake, Zainab Suleiman Omar ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa wafugaji wa samaki na wakulima wa mwani kupitia  maafisa waliogatuliwa.

Bi Zainab amesema kuwa ,  Serikali kupitia baraza la mji chake chake imedhamiria kutoa mafunzo ambayo yatatoa miongozo inayoendana na shughuli Za mazao ya bahari kwa kutambua mafanikio makubwa yanayopatikana kwa wananchi.

Maafisa ufugaji wa mazao ya baharini Muhammed Salum Othman, Aisha Bakar Masoud, wamesema kuna njia mbali mbali ambazo wafugaji wanatakiwa kuzitambua,  ili kupambana na kuepusha kutoweka kwa viumbe wanaowafuga.

Diwani wa wadi ya Kilindi, Juma Hamad Makame,  amesisitiza  wafugaji na wakulima wa mwani kujiwekea malengo wakati wa kufanya shughuli zao kwa kuzingatia taratibu zinazokubalika.

Mafunzo hayo ya siku moja kwa wafugaji wa mazao ya baharini kupitia baraza la mji Chake Chake, yanalengo la kuwashajihisha wananchi kuendeleza shughuli zao kwa utaalamu zaidi ,ili kuongeza tija na mafanikio katika ya shughuli zao.

WAKUTUBI, WATUNZA NYARAKA NA MAKUMBUSHO ZANZIBAR WAMETAKIWA KUWA NA MASHIRIKIANO

Jumuiya ya wakutubi, watunza nyaraka na makumbusho Zanzibar wametakiwa kutoa ushirikiano katika majukumu yao ya kazi kwa ajili kuondosha matatizo yanayoikibili jumuiya hiyo ili kufikia malengo ya kuitangaza kitaifa na kimataifa.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo Nd Khamis Hamad Mwitumbe ameeleza hayo katika uchaguzi wa jumuiya hiyo amesema endapo kutakuwa na ushirikiano na wanajumuiya pamoja na viongozi wataweza kufanya kazi kwa ufanisi.

Mjumbe wa jumuiya hiyo Bi Ashura Shaibu Mussa amewataka viongozi waliochaguliwa kuendelea kutoa mafunzo kwa wanachama pamoja na kuimarisha maadili ya kazi za tasnia hiyo.

Mwenyekiti watume ya uchaguzi huo Nd Kassim Salum Abdi amewataka viongozi waliochaguliwa kutekeleza yale yanayotakiwa katika jumuiya hiyo ili kufikia malengo yaliokusudia.

 

 

KMKM YAKAMATA BOTI MBILI ZIKIVUA UVUVI HARAMU

Kikosi cha kmkm kimekamata boti mbili zikivua uvuvi haramu za macho madogo katika bandari bubu ya fukuchani.

Boti hizo zimekamatwa majira ya saa nne za asubuhi zikiwa katika harakati za uvuvi huo.

Akizungumza na wavuvi hao mwanansheria kutoka idara ya maendeleo ya uvuvi zanzibar Nd Mwinyi Mataka Mwinyi amesema sheria ya uvuvi ya mwaka 2010 inakataza uvuvi haramu, hivyo vitendo vya baadhi ya wavuvi kuendelea na uvuvi wa aina hiyo ni kupingana na shehia hivyo amewakata wavuvi hao kufuata sheria za uvuvi ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza.

Mkuu wa wilaya ya kaskazini A Nd Hassan Ali Kombo amewakata wavuvi hao kubadilika na kutafuta vifaa vya uvuvi vinavokubalika ili kuweza kupata tija katika sekta hiyo.

Nao wavuvi hao wamesema wamefanya hivyo kutokana na hali ngumu ya maisha hivyo wamemtaka mkuu wa wilaya hiyo kuwasamehe.