Baraza la mawaziri limeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (vat) kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye umeme unaouzwa na shirika la umeme tanzania (tanesco) kwa shirika la umeme la zanzibar (zeco) na kufuatia malimbikizo ya deni la kodi ya vat liliofikia shilingi bilioni 22.9 kwa tanesco kwenye umeme uliozwa zeco.
WIZARA YA VIJANA ,UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO YAUNGA MKONO JITIHADA ZA VIJANA
Wizara ya vijana ,utamaduni sanaa na michezo imesema itaendelea kuunga mkono jitihada za vijana katika kuanzisha miradi inayoanzishwa na vijana hao ili waweze kupata ajira.
akifungua kikao cha utekelezaji mwenyekiti wa baraza la vijana Ndugu Khamis Hassan Kheir amesema kikao hicho kimejadili utekelezaji wa mazimio waliyoyapitishajuu ya kuanzishwa miradi ya kilimo cha hema kwa vijana katika maeneo mbali mbali ya wilaya.
Afisa mipango wa baraza hilo Ndugu Kheir Hassan Khamis amesema endapo vijana watajituma na kulima kilimo cha kisasa na kuacha kutumia kilimo cha kemikali wanaweza kuhamasisha vijana wengine kufanya shughuli za kujipatia kipato cha taifa na kupiga hatua kubwa za maendeleo Nchini.
WADAU WA MICHEZO WAJITOKEZA KUSAIDIA KLABU YA KIKWAJUNI
Wadau wamichezo wajitokeza kuisaidi klabu ya kikwajuni na kutoa ahadi ya kuisaidi klbu hiyo kurudisha makali yake kama zamani.
Akizungumza na wanachama wa klabu hiyo mdau wa michezo Mohd Raza amesema klabu hiyo watahakikisha inakuwa katika hadhi yake kwa kuisaidi na kuiwezesha kwa nyezo mbali mbali za kimichezo.
Mwenyekiti wa klabu ya kikwajuni kocha buruhani msoma pamoja na kocha wa zamanim wa timu hiyo Ibrahi Raza wamesema mashirikiano ndio ngao ya kuiwezesha timu hiyo kurudi katika makali yake.
EREA KUJADILI MASUALA YA NISHATI YA NCHI ZAO
Umoja wa wadhibiti wa mambo ya nishati Afrika mashariki erea umeanza mkutano wake hapa Zanzibar kujadili masuala ya nishati ya nchi zao hasa kutokana na kuongezeka kwa mabadiliko ya tabia nchi katika nchi hizo.
Mkurugenzi wa gesi asilia ewura tanzania Ndugu Cherles Umujuni amewaambia wandishi wa habari kwamba mkutano huo unazishirikisha mamlaka za udhibiti wa nishati hiyo za nchi wanachama wa umoja huo ambao ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Tanzania na wenyeji Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha uhusiano cha mamlaka ya huduma za maji na nishati zanzibar zura Khuzaima Ali Bakar amesema mkutano huo mbali ya kuzungumzia masuala ya nishati ya mafuta lakini pia utazungumzia masuala ya umeme, hali ya uchumi pamoja na masuala ya kisheria yanayohusu nishati hiyo.