Blog

MAHAKAMA INA MCHANGO MKUBWA KATIKA SEKTA YA UWEKEZAJI HAPA NCHINI

Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria mhe. Jaji mshibe ali bakari amesema mahakama ina mchango mkubwa katika sekta ya uwekezaji hapa nchini.

Jaji mshibe amesema hayo katika mkutano wa kupitia rasimu ya kurekebisha sheria 25 uliowashirikisha mahakimu na mawakili wa kujitegemea.

Jaji mshibe amesema wawekezaji kabla ya kuwekeza kuna vigezo wanavyotumia ikiwa ni pamoja na mwenendo wa kesi mahakamani, muda wa kesi, usimamizi wa kodi…

Hivyo amewataka mahakimu na mawakili kutumia vyema nafasi zao kwa uwadilifu na uwaminifu mkubwa katika kujenga imani kwa waekezaji kwa maendeleo ya taifa..

Ndg .mohammed khamis mwanasheria wa serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka amesema uchambuzi utasaidia kwa wale wanaozipitia  sheria kuzichambua kwa umakini  ili ziendane na zikidhi mahitaji kwa wakati uliopo..

Mwanasheria na mtafiti wa tume ya kurekebisha sheria  zanzibar ndg, nassor ameir tajo  amesema kazi inayofanyika hivi sasa sio kurekebisha sheria  bali ni kufanya utafiti na uchambuzi wa sheria katika kuhakikisha utengenezaji wa sheria bora hapa nchini

Mapema katibu wa tume ya kurekebisha sheria ndugu kubingwa mashaka simba amesema wameona umuhimu wa kujumuisha wa dau katika kafanikisha upatikanaji wa sheria bora kwa kuanzia wanasheria wa serikali mahakimu na mawakili wa kujitegemea.

 

 

 

USHIRIKIANO UNAHITAJIKA KATIKA KUULINDA NA KUUTUNZA MSITU WA HIFADHI YA TAIFA JOZANI

 

Ushirikiano wa pamoja unahitajika katika kuulinda na kuutunza msitu wa hifadhi ya taifa jozani, ili kudhibiti uharibifu wa msitu huo usiendelee kuangamizwa na kubakia kwa manufaa ya jamii na taifa .

hayo yameelezwa na mkuu wa hifadhi ya taifa jozani huba ya chwaka Bw, Ali  Ali  Mwinyi, wakati alipokuwa katika mkutano wa majadiliano ya uhifadhi wa misitu huko jozani ambapo amesema wakati umefika kwa wannchi wote wa zanzibar kupenda na kuthamini hifadhi za taifa ambazo zinasaidia kukuza pato la nchi.

mkuu huyo wa hifadhi  ameeleza kuwa hivi sasa kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuwa mlinzi wa karibu, katika kuwabaini wale wote wanaoharibu mazingira ya msitu huo kwa makusudi ili kuwachukulia hatua kali za kisheria.

mkurugenzi wa jumuiya ya uhifadhi wa mazingira jozani (jeca) bw ali juma ali, hali ni tete hivi sasa ukilinganisha na miaka iliyopita, kutokana na uharibifu mkubwa unaofanywa  na watu wasioutakia mema  msitu wa hifadhi ya taifa jozani.

nao  viongozi wa maeneo yaliyozungukwa na msitu huo wamesema wananchi wengi wamekuwa wakiutegemea zaidi msitu huo katika shughuli zao za kila siku.

WIZARA YA ELIMU KUFUTA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI

Wizara ya elimu na mafunzo ya amali zanzibar imetabgaza kufuta mitihani ya kidato cha pili iliyoanza leo, baada ya kuaminika kuwa baadhi ya watu wasiohusika kuipata baadhi ya mitihani kabla ya wakati wa kufanywa.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake amesema kitendo hicho cha kuvuja kwa mitihani kimeisabishia wizara hasara ya shilingi milioni mia mbili na hamsini na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuhusika.
Jumla ya wanafunzi 34, 848 kati yao wanaume 16, 642 wa skuli 189 za serikali na skuli 60 za binafsi za zanzibar walianza mitihani hiyo ya kidato cha pili, ambayo ilitarajiwa kumalizika jumanne ya tarehe kumi na moja.

WANAWAKE NA VIJANA WAMETAKIWA KUWAJIBIKA KWA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI NA JINSIA

Wanawake na vijana wametakiwa  kuwajibika kwa kupinga  vitendo nya ukatili na jinsia wanavyofanyiwa wanawake na watoto hapa nchini.

Mwenyekiti wa tasisi ya wanawake chakarika bi  aishaa abdulkheri muhammed amesema  wanawake wengi na watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo kwa kutokuwa na imani ingawa jamii na serikali wamekuwa wakikemea lakini bado hali hiyo imekuwa ikiendelea kwa kiwango kikubwa

Hvyo kwa kupitia mafunzo hayo wanaharakati hasa vijana wameombwa kuitumia vyema elimu hiyo kwa kukomesha .

Wakufunzi wa mafunzo hayo wamewaomba waliopatiwa mafunzo hayo kuyatumia kwa kufikisha ujumbe kwa jaamii ili kuachana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji.

Washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kutoa elimu hiyo kwa jamii kwani vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka kwa idadi kubwa .