NGUZO ZA UMEME KUTOKA FUMBA KUELEKEA MTONI ZIPO HATARANI

 

Baadhi ya nguzo za umeme za njia kuu ya umeme kutoka fumba kuelekea mtoni zipo hatarani baada ya mvua zinazoendelea kusababisha mmongonyoko wa ardhi shehia ya karakana.

Mmaongonyoko huo unadaiwa kusababishwa na   kiwango kikubwa cha maji kupita karibu na nguzo hizo baada kuharibika kwa mtaro

Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamesema  hali ilivyofikia inawatia wasiwasi wa maisha yao kwani nguzo hizo zinazopitisha umeme mkubwa iwapo zitaanguka zitafika hadi katika nyumba zao.

Wameiomba  shirik la umeme zanzibar zeco kuchukuwa hatua za haraka kunusuru hali hiyo kwa kutafuta ufumbuzi wa haraka pamoja na kuomba mansipaa kufanyia matengenezo mtaro wa eneo hilo ulioharibika kwa kipindi kirefu.

Afisa    uhusiano  wa    zeco   salum  abdalla   amesema   italifanyia  kazi  suala  hilo  na   kuwataka    wananchi   kutoa taarifa mapema wanapobaini  kasoro za miundo mbinu ya  umeme kwa ajili ya usalama wa maisha yao.