NIGERIA YATHIBITISHA WASICHANA 110 HAWAJULIKANI WALIKO

 

 

Serikali ya nigeria imethibitisha kuwa wasichana 110 hawajulikani waliko baada ya kundi la boko haram kushambulia skuli kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wiki iliyopita.Serikali ya Nigeria ilikuwa haijasema lolote kuhusiana na kutoweka kwa wasichana hao.Hatua ya kutekwa nyara kwa wasichana hao imeibua maswali kuhusu tamko la mara kwa mara la jeshi la Nigeria kwamba kundi la Boko Haram linaelekea kuangamizwa baada ya miaka 9 ya kupambana nalo vikali.Utekaji huo umezifufua kumbukumbu za mwaka 2014 ambapo zaidi ya wasichana 200 wa skuli walitekwa nyara eneo la Chibok.Ijumaa iliyopita rais muhammadu buhari aliziomba radhi familia za wasichana waliotoweka akisema ni janga la kitaifa.