NJIA PEKEE YA KUHAKIKISHA TUNAKUA SALAMA NCHINI NI KUVITOLEA TAARIFA VITENDO VYA RUSHWA NA UHUJUMU WA UCHUMI

 

njia pekee ya kuhakikisha tunakua salama nchini ni kuvitolea taarifa vitendo vya rushwa na uhujumu wa uchumi  Zanzibar.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Elimu kwa Umma Sheha Kombo Hamadi wa kati akiwafahamisha wananchi wa shehia ya uroa katika tawi la CCM.

Amesema kufanya hivyo itasaidia kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Kushirikiana na ZAECA katika kuwafichua wanaaojihusisha na vitendo hivyo bila ya kuoneana aibu na muhali ili kuwa na maendeleo endelevu.

Nao  wananchi wa shehia hiyo wameiomba  ZAECA kuzidisha juhudi ya kutoa elimu kwa jamii, viongozi, kuweka mitaala ya elimu kwa wanafunzi, pia kila shehia kuweka watu maalum ambao watasaidia kudhibiti vitendo hivyo.