NYUMBA ISHIRINI NA SITA ZINAHITAJI KUFANYIWA MATENGENEZO ZA MJI MKONGWE
Jumla ya nyumba ishirini na sita zinazomilikiwa na shirika la nyumba zilizomo katika mji mkongwe zimebainika kuwa zinahitaji kufanyiwa matengenezo ili kuyaweka salama maisha ya wakaazi wake.
akizungumza katika ziara ya kukagua nyumba hizo iliyofanywa na mkuu wa wilaya ya mjini Marina Joel Thomas, katika shehia ya mkunazini, mkurugenzi mkuu shirika la nyumba Nd. Mohammed Hafidh, amesema nyumba hizo zinakabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ya ubovu wa kupasuka kwa kuta jambo linalohatarisha usalama wa wakaazi wake.
amesema kwa hatua ya kwanaza kiasi cha shilingi billion 12 zinahitajika kuzifanyia matengenezo ili kuzirudishia haiba yake nyumba hizo.
nae mkuu wa wilaya ya mjini Marina Joel Thomas amesema ziara hiyo ina lengo la kutaka kujua hali halisi ya usalama wa wakaazi,ulipaji wa kodi,mikataba kwa waazi hao pamoja na utunzaji wake
baadhi ya nyuma hizo zimekuwa zikitumika kwa shughuli za kibiasha na makaazi.