OMAN KUTOA USHAURI NA MSAADA KWA ZANZIBAR JUU YA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI

Waziri wa mafuta na gesi wa oman mohammed ahmed al – ramhy ameeleza kufurahishwa na taarifa ya zanzibar kutaka kuchimba mafuta na kusema kwamba serikali ya oman iko tayari kutoa ushauri na msaada kwa zanzibar katika kutimiza azma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada kukamilisha ziara yake ya siku moja kisiwani pemba amesema pamoja na kwamba zanzibar na oman itakuwa kuna njia tofauti za uchimbaji mafuta lakini serikali yake itakuwa tayari kutoa kila aina ya ushauri ili kuona kwamba kazi hiyo inafanywa kwa ufanisi.
Akizungumzia hali halisi ya watu wa zanzibar hakusita kueleza kufurahishwa kwake na hali ya ukarim wa wakaazi wa kisiwani pemba na zanzibar kwa ujumla na kueleza kwamba hali hiyo ni kielezo tosha cha kuwavutia wageni wakiwemo watalii kufika zanzibar.
Katika ziara yake hii akiambatana na viongozi mbali mbal i wa serekali waziri huyo ametembelea skuli ya uweleini, hospitali ya abdalla mzee mkoani, bandarini mkoani pamoja na msitu wa ngezi ambapo hapo alipewa maelezo kidogo kuhusiana na vivutio vilivyomo kwenye msitu huo.