OPERATION MAALUM YA SAFISHA KIWENGWA INA LENGO LA KUDUMISHA AMANI

 

 

Mkuu wa wilaya ya kaskazini b ndugu rajab ali rajab amefanya kikao maalum na mapapasi wanaofanya shughuli zao katika fukwe ya kiwengwa ikiwa ni muendelezo wa operation maalum  ya safisha kiwengwa ambayo ina lengo la kudumisha amani kwa watalii pamoja na wawekezaji

Amesema lengo la kikao hicho ni kudhibiti  matukio mbalimbali  ambayo yamekuwa yakijitokeza katika shehiya hiyo ikiwemo kupora mali za watalii  ambapo ni viashiria vya na  kuzorotesha kwa shughuli za kitalii katika eneo hilo

Hayo ni baadhi ya matukio ambayo yamekuwa yakiwakuta watalii ambapo mkuu wa wilaya ya kaskazini b ameahidi kuyafanyia kazi kwa kuendelea na operation hiyo ili kuweka usalama kwa wawekezaji na watalii ambao wamekuwa wakiingizia mapato serikali.

Amesema kutokuwepo kwa usimamizi mzuri kutoka kwa viongozi wa makundi ya mapapasi hao na kusema serikali ya wilaya  itahakikisha inasimamia taratibu za utendaji kazi pamoja na kuweka vitambulisho maalum vitakayoonesha shughuli anazofanya papasi katika fukwe hiyo

Sheha wa shehiya ya kiwengwa ndugu mauled massoud ame amesema baadhi ya hatua alizozichukua katika kukabiliana na tatizo hilo

Kwa upande wao mapapasi hao wamemuelezea mkuu huyo wa wilaya   matatizo wanayokutana nayo kutoka kwa baadhi ya hoteli  ambazo zinawafanyia usumbufu kwa kuhitaji malipo pindi wanapoingia katika fukwe hali ambayo inawapa usumbufu pamoja na kuushauri uogozi wa wilaya kutoa elimu ya usalama kwa walinzi

Katika hatua nyengine mkuu huyo wa wilaya amewataka wamiliki wa baa ya peru na vision kupiga mziki kwa kufuata  utaratibu uliowekwa ambao ni kuanzia siku ya ijuuma hadi jumapili saa 12  jioni mpaka saa 6 usiku ili kuondoa usumbufu kwa wakaazi wa maeneo ya karibu na baa hizo kabla ya kuchukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa kwa baa hizo.