PBZ ITAPANUA UTOAJI WA HUDUMA ZAKE ZA KIFEDHA ILI KUJIIMARISHA KIUCHUMI

 

 

Benki ya watu wa zanzibar pbz  imesema itapanua utoaji wa huduma zake za kifedha ili kujiimarisha kiuchumi sambamba kuwadhirisha wateja wake katika maeneo mbali mbali nchini.Akizungumza  katika  maadhimisho ya miaka 52 tokea kuanzishwa kwa benki hiyo  mkurugenzi mtendaji wa benki ya watu wa zanzibar bw juma ameir hafidh  amesema  huduma hizo zitaendeshwa kwa njia ya uwakala mjini na vijijini. Amewataka wananchi  kujitayarisha na utoaji wa huduma hizo kupitia  njia ya uwakala hatua itakayosaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Naibu mkurugenzi  mtendaji wa pbz bi khadija shamte mzee  amesema kwa sasa benki hiyo ipo katika mpango wa kuanzisha visa kad ambayo itawawezesha wateja wao kupata huduma hiyo popote pale walipo nje na ndani ya nchi sambamba na kuongeza huduma ya mashine za atm ili kuwarahisishia  huduma  wateja wao. Nao baadhi ya wateja wa benki hiyo wameelezea kuridhishwa na  huduma wanazozipata kutoka benki hiyo huku wakishauri  kupatiwa ufumbuzi matatizo yanayowasumbua wateja wa benk hiyo.