POLISI NCHINI MALAYSIA WAGUNDUA KILICHOMUUA KIM JONG NAM

 

Polisi nchini malaysia wamesema kuwa wamefichua kemikali iliyotumika kumuuwa ndugu wa kiongozi wa korea kaskazini kim jong-nam.

Wamesema kuwa vx dawa ya neva ambayo ni sumu kali inayotumika katika vita vya kemikali.

Korea kaskazini wiki iliyopita ilisema kuwa haitambui matokeo yeyote yatakayotokana na uchunguzi wao na kutaka warejeshewe mwili.

Kim jong-nam aliuwawa katika shambulio hilo la sumu, kwenye uwanja wa ndege wa kuala lumpur, mapema juma lililopita.