POLISI NCHINI URUSI WAMEWAKAMATA ZAIDI YA WATU 200 WALIOKUWA WANAANDAMANA

Polisi nchini urusi wamewakamata zaidi ya watu 200 waliokuwa wanaadamana katika maadhimisho ya tarehe ya kuzaliwa rais wa urusi vladimir putin.
Polisi hao wamechukua hatua kali katika mji alikozaliwa rais huyo wa st. Petersburg kujaribu kuyazima maandamano ya watu wapatao elfu tatu ambayo hayakuruhusiwa.
Katika mji mkuu wa urusi, moscow, maandamano ya watu elfu moja yalifanyika lakini kwa kiwango kikubwa yalikuwa ya amani.
Maandamano hayo yalifanyika kuitikia mwito alioutoa kiongozi wa upinzani kuwashinikiza viongozi wa serikali ya urusi wamruhusu kushiriki katika kinyang’anyiro cha kugombea urais.
Kiongozi huyo kwa sasa anatumikia kifungo cha siku 20 jela kwa kosa la kuitisha maandamano ambayo hayakuruhusiwa.