POLISI YA AUSTRALIA YAZIMA JARIBIO LA KIGAIDI LA KUIDUNGUA NDEGE

Polisi nchini Australia imezuia njama ya kuidungua ndege kwa kutumia milipuko na kuwakamata watu wanne, baada ya kufanya misako majumbani katika viunga kadhaa vya mji wa Sydney.
Waziri Mkuu Malcom Turnbull amesema usalama umeimarishwa katika uwanja wa ndege wa Sydney tangu siku ya Alhamisi kwa sababu ya njama hiyo.
Hatua hizo zilizoimarishwa za usalama pia zimewekwa kwenye viwanja vyote vya safari za kimataifa na za ndani kote nchini Australia jana usiku.
Mashambulizi kadhaa ya kigaidi yametokea Australia katika miaka ya karibuni, ikiwa ni pamoja na uvamizi wa mkahawa mmoja mjini Sydney mwaka 2014 ambako wateja wawili waliuwawa, polisi mmoja wa Sydney na mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 15.