PUTIN AAGIZA WANADIPLOMASIA 755 WA MAREKANI KUONDOKA URUSI

Rais wa urusi vladimir putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa marekani nchini urusi kusitisha shughuli zao kufikia septemba mosi mwaka huu.
Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana.
Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo.
Rais huyo wa urusi amesema upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya marekani.
Urusi imekuwa ikikanusha kuingilia kwa vyovyote uchaguzi huo.