QATAR IMEKANA KUUNGA MKONO MASUALA YA KIGAIDI

Qatar imekana kuunga mkono masuala ya kigaidi na wametaka kuwepo mazungumzo kuhusu tuhuma hizo.
Serikali ya nchi hiyo imesema mzozo huo hautaathiri utaratibu wa maisha , ingawa kuna taarifa za wananchi kuanza kuhifadhi chakula kama dharura tangu mzozo huo ulipoibuka mapema wiki hii.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa qatar sheikh mohammed bin abdulrahman al-thani, amesema ndege zake zinatumia njia za kimataifa za baharini kwa safari za kimataifa.
Wakati huo huo sudan imejitolea kuchukua nafasi kama mpatanishi wa kutatua mgogoro unaoendelea, kati ya qatar na mataifa mengine ya kiarabu.