QATAR IMETAKA MAZUNGUMZO NA NCHI ZILIZOIWEKEA VIKWAZO

 

Waziri wa mambo ya nje ya russia sergio lavrov amefanya mkutano na mwenzake wa qatar sheikh mohammed bin abdulrahman al thani kwa waandishi wa habari nchini qatar.

Sheikh al thani amesema serikali ya qatar tayari imetaka mazungumzo na nchi zilizoiwekea vikwazo nchi hiyo ambapo hadi sasa nchi hizo hazijatoa majibu ya kukubali ama kukataa mazungumzo hayo.

Saudi arabia, umoja wa falme za kiarabu, bahrain na misri bado hazijatoa majibu yeyote ikiwa ni dalili ya kuonesha ushirikiano hafifu na kutaka kuendeleza mgogoro huo wa ghuba.