QATAR YALAANI VIKWAZO DHIDI YAKE

Qatar imelaani vikwazo ilivyowekewa na saudi arabia na washirika wake na kuvitaja kuwa visivyo vya haki na vinavyokiuka sheria.
Waziri wa mambo ya nje sheikh mohammed bin abdulrahman al-thani, akiwa ziarani mjini paris, ametoa mwito wa kufanyika kwa majadiliano ya wazi, kuhusiana na tuhuma kwamba qatar inaunga mkono makundi ya itikadi kali.
Mjini london, waziri wa mambo ya kigeni wa uingereza boris johnson pia alitoa wito wa utulivu na kusema atakutana na wenzake kutoka saudi arabia, kuwait na umoja wa falme za kiarabu.
Waziri wa ulinzi wa marekani jim mattis amesema mzingio dhidi ya qatar unaweka hali ngumu na kutoa rai kwa washirika hao wa ghuba kutatua mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo.