RAIA 100 WAMEKUFA KUFUATIA MASHAMBULIZI YA ANGANI YALIYOFANYWA NA VIKOSI VYA SYRIA

 

 

Zaidi ya raia 100 wamekufa kufuatia mashambulizi ya angani yaliyofanywa na vikosi vya syria na urusi katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi mashariki mwa ghouta katika siku ya pili ya mashambulizi hayo.

Ikiwa ni hatua kubwa katika vita vilivyodumu kwa miaka saba nchini syria, pia imetuma wanajeshi damascus wanaoiunga mkono serikali katika eneo la kaskazini mwa afrin ambako wamekabiliana vikali na majeshi ya uturuki yanayopambana katika eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa kikurdi.

Shirika linaloshughulikia haki za binaadamu nchini syria limesema takriban raia 250 wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi siku ya jumapili na idadi kubwa ni watoto.Mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa siku ya jana yamesababisha vifo vya raia zaidi ya 100 miongoni mwao ni watoto 9.