RAIA 15 WAUAWA KATIKA MASHAMBULIZI YA ANGA LIBYA

kiasi ya watu 15 wameuwawa katika mashambulio ya anga katika mji wa mashariki mwa Libya wa Derna. Kiasi ya watu 17 wamejeruhiwa ambao wote ni raia wengi wakiwa na wanawake na watoto. Derna ni mji ambao umekuwa kwa muda mrefu katika mzingiro wa jeshi lililoko upande wa mashariki la libyan national army ambalo mara kwa mara hufanya mashambulizi ya anga dhidi ya mji huo. Maafisa wa jeshi wamekataa kusema lolote kuhusu mashambulizi hayo.