RAIA WA UJERUMANI KUJERUHIWA.BAADA YA AJALI MKOA KASKAZINI

 

 

Ajali ya gari imetokea maeneo ya kazole mkoa wa kaskazini unguja baada gari mbili kugongana uso kwa uso na kusababisha mtu mmoja raia wa ujerumani kujeruhiwa.

Zbc ambayo imeshuhudia ajali hiyo iliyozihusisha gari aina ya noah yenye namba za usajili 2793 ya island express kugongana na gari aina ya canter ambapo dereva wa gari hiyo amekimbia.

Dereva wa gari ya noah aliyejitambulisha kwa jiana la haji mohamed ambae gari yake imechukuwa watalii amesema alikuwa akitokea mjini kuelekea nungwi na ndipo gari ya mizigo canter ikapoteza mwelekeo na kumgonga.

zbc imetafuta kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini unguja hassina ramadhan taufik amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusema kuwa majeruhi wametibiwa na kuruhusiwa huku jeshi pla polisi likichunguza chanzo cha ajali hiyo.

Wananchi waliokaribu na eneo lililotokea ajli wameiomba serikali kuweka matuta katika eneo hilo kwani limekuwa likitokea ajali za mara kwa mara.