RAIS BUHARI AREJEA NYUMBANI AMALIZA UVUMI KUHUSU AFYA YAKE.

 

Rais wa nigeria muhammadu buhari amerejea nchini mwake, baada ya kuwa nje ya nchi kwa wiki kadhaa, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu nchini uingereza.

Buhari mwenye umri wa miaka 74, ambaye alichukua madaraka ya nchi hiyo mei, 2015 aliondoka mjini abuja januari mwaka huu, kwaajili ya matibabu nchini uingereza. Hata hivyo taarifa ya ikulu haikuweka wazi kuhusu kilichokuwa kikimsumbua rais buhari.

Serikali ya nigeria imekuwa ikijaribu kuwatoa hofu wananchi wa nigeria ambao walikuwa na wasiwasi kuhusu mwenendo wa uchumi wa taifa hilo wakati rais buhari akiwa nje ya nchi.