RAIS DONALD TRUMP AMESIFU UKUAJI WA UCHUMI WA MAREKANI

 

Rais donald trump amesifu ukuaji wa uchumi wa marekani, kiwango cha chini cha ukosefu wa ajira na ongezeko la mishahara katika hotuba yake ya kwanza ya hali ya taifa hilo.

Pia amezungumzia kanuni muhimu ya kisiasa, ikiwa ni mageuzi ya uhamiaji, ambayo ni pamoja na kulinda mipaka ya marekani na kusitisha mfumo wa kupata viza kwa njia ya bahati nasibu.Katika hotuba yake hiyo ya dakika 80 amesema marekani inahitaji kuwa ya kisasa zaidi na kujenga upya hazina yake ya silaha za kinyuklia, lakini amesema haina nia ya kuzitumia.

Pia amezitaja china na urusi kuwa nchi ambazo zinatoa changamoto kwa maadili ya marekani.Akizungumzia kuhusu kupunguza kodi na ukiritimba, kiongozi huyo alishangiriwa mara kadhaa na wabunge wa chama cha republican, wakati wabunge wa chama cha upinzani cha democratic walipokea miito yake mingi kwa kukaa kimya.