RAIS DONALD TRUMP WA MAREKANI AMEAPA KUIANGAMIZA KABISA KOREA KASKAZINI

Rais donald trump wa marekani ameapa kuiangamiza kabisa korea kaskazini iwapo marekani italazimika kujihami au kuwalinda washirika wake dhidi ya mpango wa kinyuklia wa korea kaskazini.
Akizungumza kwa mara ya kwanza katika kikao cha baraza kuu la umoja wa mataifa tangu kuingia madarakani, trump amezishutumu nchi kadhaa zikiwemo korea kaskazini na iran, kuwa ni tawala zenye uchokozi kwa kusema kiongozi wa korea kaskazini kim jong un anapaswa kuzuiwa kuendelea na mpango hatari wa kinyuklia unaotishia ulimwengu mzima.
Hotuba hiyo imeibua hisia tofauti kutoka kwa viongozi kadhaa wa dunia ambapo waziri mkuu wa israel benjamin netanyahu ameisifu hotuba hiyo huku waziri wa mambo ya nje wa iran javad zarif akiikosoa na kusema sio inayotarajiwa katika karne hii ya 21 na haistahili hata kujibiwa.