RAIS DONALD TRUMP WA MAREKANI AMEITILIA SHAKA NIA YA ISRAEL YA KUPATANA NA WAPALESTINA

 

 

Rais donald trump wa marekani ameitilia shaka nia ya israel ya kupatana na wapalestina akisema ujenzi wa makaazi katika ukingo wa magharibi ni jambo linalozidi kuvuruga mchakato huo.

Katika mahojiano yaliyochapishwa jana katika gazeti la   nchini israel, trump pia ameelezea mashaka yake kuhusiana na nia ya palestina kuhusiana na kupatikana mwafaka.Lakini matamshi yake ya kuikosoa israel ndiyo yanayochukuliwa kwa uzito kutokana na kuwa amekuwa na uhusiano mzuri na israel, huku akizozana na palestina kabla kuwasilishwa kwa ule mpango unaotarajiwa wa amani wa marekani.Gazeti hilo la israel linamilikiwa na bilionea wa marekani,   ambaye anamuunga mkono trump na ni mfuasi wa waziri mkuu wa israel, benjamin netanyahu.