RAIS DONALD TRUMP WA MAREKANI AMEONYWA NA WANACHAMA WA CHAMA CHAKE

 

Rais donald trump  wa marekani ameonywa na wanachama wa chama chake cha republican kuacha kuingilia uchunguzi maalumu kuhusiana na urusi kuingilia uchaguzi wa marekani uliopita.Hatua hii ya wanachama wa republican inakuja baada ya rais trump kumshambulia kuhusiana na uchunguzi wake dhidi ya urusi kudaiwa kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.

Ktika ukurasa wake wa twitter mwishoni mwa  wiki hii trump alirejea kutoa utetezi wake akisisitiza kuwa hakukuwa na uhusiano wowote kati ya timu yake ya kampeni na urusi na kusema kuwa hiyo ni vita binafsi inayoshabikiwa na democrats.Mueller,ambaye ni mkuu wa zamani wa fbi, anaungwa mkono na republican kuendelea na uchunguzi wake bila kuingiliwa.Senata lindsey graham amesema trump asijaribu kuchukua hatua yoyote dhidi ya mueller ikiwemo kujaribu kumfukuza  kazi.