RAIS DONALD TRUMP WA MAREKANI AMEWASILI NCHINI ISRAEL

Rais Donald Trump wa marekani amewasili nchini israel akitokea saudi arabia ambapo amesema eneo la mashariki ya kati lina fursa muhimu kupata amani.
mara baada ya kuasili nchini humo Trump amepokelewa na mwenyeji wake waziri mkuu Benjamin Netanyahu alielezea kuwa ziara hiyo kuwa ni hatua ya kihistoria kuelekea amani na maridhiano.
hapo kesho rais Trump anatarajiwa kutembelea maeneo ya wapalastina yanayokaliwa na isarael katika ukingo wa magharibi, na atazungumza na rais wa palestina mahmoud abbas.
hii ni sehemu ya pili ya ziara yake ya kwanza nje ya marekani iliyoanzia nchini saudi arabia tangu alipoingia madarakani mwezi januari.