RAIS KENYATTA AMEKATAA KUKUTANA NA CHEBUKATI NA AMEENDELEA NA KAMPENI

 

 

Mkurugenzi mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini kenya ezra chiloba, amesema anakwenda likizo kwa muda wa wiki tatu licha ya upande wa upinzani kutaka ang’atuke kabla ya uchaguzi wa rais kuitishwa upya oktoba 26.

Anasema ameamua mwenyewe kuchukua likizo hiyo na ameongeza kuwa kila kitu kimeandaliwa vizuri kwa ajili ya uchaguzi kama ilivyoamriwa na mahakama kuu.

Upande wa upinzani unaoongozwa na raila odinga umesema unasusia uchaguzi mpya hadi madai yao yatimizwe ikiwa ni pamoja na kutolewa kazini mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wafula chebukati.

Jana odinga amekutana na chebukati na kuwaambia waandishi wa habari kuwa upande wa upinzani unaweza kuzingatia upya msimamo wake ikiwa mageuzi na ushauriano ya dhati yatafanyika ambapo rais kenyatta amekataa kukutana na chebukati  na ameendelea na kampeni.