RAIS MTEULE WA COLOMBIA IVAN DUQUE AMETOA WITO WA KUWEPO UMOJA NCHINI HUMO

 

Rais mteule wa colombia ivan duque ametoa wito wa kuwepo umoja nchini humo baada ya kushinda katika duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mwanasiasa wa mrengo wa kushoto gustavo petro.

Mhafidhina duque amechaguliwa kwa asilimia 54 ya kura na anakuwa kiongozi wa colombia mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuliongoza taifa hilo la amerika kusini.

Ameahidi kufanya kila juhudi kuondoa migawanyiko na pia kukabiliana na ufisadi na biashara ya cocaine.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 41 amesema kila mmoja anataka kuona amani nchini colombia lakini makubaliano ya amani yaliyofikiwa na mtangulizi wake rais juan manuel santos mwaka 2016 yanahitaji kufanyiwa marekebisho, ili waathiriwa wa mzozo uliodumu miaka 52 nchini humo waweze kupata haki.

Jambo amblo limesababisha wasiwasi kuhusu hatima ya makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya serikali na kundi la zamani la waasi farc