RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMEKUTANA NA MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA

 

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amekutana na mwakilishi wa Benki ya dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia.

Mwakilishi huyo Bi. Bella Bird amemhakikishia Rais Magufuli kuwa benki hiyo imejipanga kuendelea kutoa mikopo nafuu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ili kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Amebainisha maeneo ya kipaumbele kuwa ni miundombinu barabara na reli, kuongeza uzalishaji na usambazaji wa nishati ya umeme, teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) na elimu huku akisifu usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na benki ya dunia.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameishukuru Benki ya dunia kwa ushirikiano wake na Tanzania katika maendeleo na amemhakikishia mwakilishi huyo kuwa serikali itazisimamia vizuri fedha zinazotolewa na benki hiyo.