RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

 

Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania mh. John pombe magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa, makatibu wakuu,  makatibu  tawala na manaibu aliowateuwa hivi karibuni.

Halfa hiyo ya uapisho imefanyika ikulu jijini dare s salaam na kuhudhuriwa na makamo wa rais mama samia suluhu hassan, waziri mkuu kassim majaaliwa, mawaziri, manaibu waziri ,viongozi wa dini na vyama vya siasa ambapo walioapishwa ni pamoja na mkuu wa mkoa wa iringa ally salum hapi, mkuu wa mkoa wa kagera brigedia jenerali marco elisha kaguti, mkuu wa mkoa wa mbeya albet  chalamila, na mkuu wa mkoa wa songwe nikodemas elias mwangela.

Wengineo ni profesa joseph buchweshahija katibu mkuu wa wizara ya viwanda biashara na uwekezaji, andrew wilisom masawe katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu sera bunge kazi vijana na watu wenye ulemavu, profesa elisante ole gabriel katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi anayeshughulikia mifugo, na manaibu katibu wakuu wawili, makatibu tawala wa mikoa 13,  na manaibu  katibu tawala wawili.

Akizungumza katika hafla hiyo  rais  magufuli amewataka watendaji hao  kwenda kujenga mahusiano mazuri  na wanaowaongoza pamoja na kuzitafutia ufumbuzi kero na changamoto zinazowakabili wananchi   pamoja na  kusimamia kwa ukamilifu  ukusanyaji wa mapato  kwenye halmashauri.

Nae makamo wa rais mhe samia  suluhu hassan amewataka viongozi walioapishwa kwenda kusimamia viapo vyao kikamilifu kwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha za umma, na kuzikabili changamoto za wananchi na sio kungojea mpaka viongozi wakuu wafike eneo husika.

Waziri mkuu kassimu majaliwa akawataka watendaji hao kufanya kazi kwa uadilifu ili kukamilisha malengo ya serikali.

Mara baada ya kuapishwa viongozi hao walikula kiapo cha uadilifu zoezi lililoongozwa na jaji mstaafu aron sekela.