RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI WAWILI

Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania mh. Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha mawaziri wawili kufuatia mabadiliko madogo  aliyoyafanya katika baraza la mawaziri pamoja na kumuapisha balozi wa Tanzania nchini malawi..

 halfa hiyo ya uapisho imefanyika ikulu jijini Dare s salaam na kuhudhuriwa na waziri mkuu kassim majaaliwa, ,jaji mkuu wa tanzania prof.ibrahimu khamis, spika wa bunge job ndugai, katibu mkuu kiongozi balozi john kijazi ,viongozi wakuu wa vyomba vya ulinzi  na usalama, mawaziri, manaibu waziri ,viongozi wa dini na vyama vya siasa.

mawaziri walioapishwa ni Profesa Palamagamba kabudi waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki, na  waziri wa katiba na sheria mhe balozi dk. Augustine mahiga.

Aidha Rais Magufuli amemuapisha Hassan Simba kuwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini malawi..

Akizungumzia kuhusu rais magufuli amesema mabadiliko hayo aliyoyafanya, kuwa ni ya kawaida .

Na kuhusu jeshi la polisi rais magufuli    amesema anathamini  kazi inayofanywa na jeshi hilo kwani linafanya kazi vizuri licha kuwepo kwa kasora ndogo ndogo,  na akalitaka kuziondosha kasoro hizo .

Katika hatua nyengine rais magufuli akazungumzia kusikitishwa kwake na upelelezi juu ya kutekwa kwa mfanyabiashara mohammed dewji ( mo ) na kusema  ukimya huo umeacha maswali mengi.

Naye waziri mkuu mhe kassim majaliwa amewapongeza mawaziri walioteuliwa na kusema kuwa ni imani yake kuwa watafanya kazi                                                                                                                                           kwa umahili kutokana na uzoefu wao, na akamtaka balozi aliye apishwa  kwenda kusimamia mahusiano mazuri baina ya tanzania na malawi .

Kwa upande wao mawaziri  waliokula kiwapo  walikuwa na haya ya kusema.

Aidha katika hafla hiyo mkuu wa jeshi la polisi igp simon sirro amewapandisha vyeo manaibu makamishina watano wa jeshi hilo kuwa makamishina.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App