RAIS WA JIMBO LA CATALONIA PUIGDEMONT YUKO UBELGIJI

Rais wa jimbo linalotaka kujitenga nchini uhuspania la catalonia carles puigdemont yuko ubelgiji ambako ameomba msaada wa kisheria.
wakili wa kiongozi huyo amesema amekutana binafsi na puigdemont.
mwanasheria mkuu wa serikali ya uhispania jose manuel maza hadi sasa hajafungua mashitaka dhidi ya puidgemont na viongozi wenzake wa jimbo hilo.
maza amesema kwamba shutuma dhidi ya watuhumiwa ni pamoja na uasi, mapinduzi dhidi ya mamlaka ya serikali na matumizi mabaya ya fedha za umma.
wakati huo huo kiongozi huyo amezungumza na waandishi wa habari mjini brussels kuhusu hatua yake ya kuikimbia hispania.
uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya jimbo la katalonia kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba.
hata hivyo serikali kuu ya hispania imechukua uamuzi wa moja kwa moja kutangaza kuiongoza serikali ya katalonia kupitia serikali kuu.