RAIS WA KOREA KUSINI AONDOLEWA MADARAKANI

 

Mahakama ya kikatiba ya korea kusini imetoa uamuzi wa kuufikisha mwisho utawala wa rais park geun hye aliyeshitakiwa na bunge la nchi hiyo.

Bunge hilo lilimshitaki park mwezi desemba mwaka jana kwa kutumia vibaya madaraka na ufisadi baada ya mamilioni ya watu kuandamana wakimtaka rais huyo ajiuzulu kufuatia kashfa mbalimbali za ufisadi na rushwa.

Uamuzi huo uliofikiwa na jopo la majaji nane wa mahakama ya kikatiba ambao hauwezi kukatiwa rufaa unamaanisha korea kusini itafanya uchaguzi katika kipindi cha miezi miwili ijayo kumchagua rais mpya.

Park mwenye umri wa miaka 65, ni mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo na kiongozi wa kwanza kuondolewa madarakani.