RAIS WA MAREKANI DONALD TRUM AMEPUUZA TAARIFA ZILIZOUTIKISA UTAWALA WAKE

Rais wa marekani donald trump amepuuza taarifa zilizoutikisa utawala wake baada ya aliyekuwa mshauri wake wa usalama wa ndani michael flynn kukiri kwamba aliwadanganya maafisa wa shirika la upelelezi fbi, na kuahidi kwamba atashirikiana na mwanasheria maalum anayechunguza iwapo urusi iliingilia uchaguzi wa rais wa marekani.
Trump amesisitiza kuwa yeye na timu yake hawakushirikiana na urusi kuuingilia uchaguzi na alimfuta kazi mshauri huyo kwa sababu alimpotosha makamu wa rais mike pence na shirika la fbi.
Wakati flynn alipofutwa kazi, ikulu ya marekani ilisema kwamba alimdanganya makamu wa rais wala si fbi hivyo uhusiano wa rais trump na mshauri wake wa zamani wa masuala ya usalama wa taifa unachunguzwa tangu aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la upelelezi la marekani fbi, james comey alipofutwa kazi mwezi mei, mwaka huu.